Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima amesema takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa wanaume ndio vinara wa vitendo vya ukatili kwa . watoto katika matukio ya ulawiti na ubakaji .
Alisema kuwa kati matukio 12,100 ya ukatili ya ,matukio 10000 wamefanyiwa watoto wa kike huku matukio 6000 ni ubakaji na matukio 1500 watoto wa kiume walilawitiwa.
"Ninyi kina baba jiulizeni na mjitafakari, mnakubalije kubeba hii dhambi na hii laana "
Aliwataka wanaume wakae chini na kujitafakari na kuwataka watazeme upya hizo takwimu za ukatili zinasababishwa na nini ama ni ushirikina afya ya akili ,malezi mabaya au ukosefu wa maadili.
Aliwashauri wanaume watazame upya ili wanawake waishi kwa amani kwani wanapambana na majukumu mengi ikiwemo cha changamoto za kifamilia , uwezo mdogo wa kipato ,elimu na ujuzi duni, mila na desturi kandamizi.
Dkt Gwajima ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi kijijini yaliyofanyika Kijiji cha Olevolos, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha yenye kauli mbiu isemayo “Wezesha Wanawake Wanaoishi Kijijni Kwa Uhakika wa Chakula ,Lishe na Uendelevu wa Familia”
Alisisitiza wanawake kuendelea kuzalisha zaidi chakula ili kuhakikisha lishe zinapatikana ndani ya familia ingawa wanawake wanaonewa na matukio ya ukatili ,kunyanyaswa na mila za kitamaduni ambazo baadhi ya makabila mwanamke hapewi nafasi katika maamuzi.
Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru,Emanuela Kaganda aliwataka wadau wa maendeleo kuwekeza sekta ya mikopo wilayani huo ili kuwapatia mikopo nafuu wanawake wajasirimali waepukane na mikopo kausha damu ambayo imekuwa kichocheo cha umasikini.
"Kuna wanawake wengi wanakuja ofisini kwangu wakiwa na watoto wadogo wamekimbia familia zao na wameacha watoto sababu ya mikopo ya kausha damu ,nitumie fursa hii kuwaalika wadau wa sekta ya mikopo nafuu kuja kuwekeza katika wilaya yangu ili kuwasaidia akina mama hao"
Naye mwenyekiti wa ccm wilaya hiyo Noel Severe alisema hali ya unyanyasaji kwa wanawake na watoto wilayani humo bado ni kubwa na kuwataka wanaume washiriki ipasavyo katika kupambana na kupinga vitendo hivyo.
"Kuna janga la unyanyasaji wa kijinsi unaendelea hasa ulawiti kwa watoto wa kiume jambo hilo halina chama, dini , jinsia ,rika wala kabila ni jambo letu some tushirikiane sote tukitumua mila zetu kupambana na janga hilo"
Baadhi ya wadau wanaopambana na ukatili katika jamii ,Rajab Suedy kutoka Sumaujata alisema hali ya ukatili vijijini ni kubwa ikiwemo wanaume kufanyiwa ukatili na wenzao wao akidai hali hiyo inatokana na hali duni ya maisha na umasikini.
Alisema kupitia maadhimisho hayo wanawake watapata elimu ya kujitambua ili kupaza sauti zao pale wanapokumbana na ukatili wa aina mbalimbali
Awali mwathirika wa tukio la ukatili,Mwalimu Veronica Kidemi mkazi wa sekei ambaye aliwasisimua na kuwatoa machozi wananchi alidai kufanyiwa ukatili kwa kukatwa kiganja cha mkono na mume wake mwaka 2020 .
Aliishauri serikali kuanzisha mahakama itakayoshughulikia masuala ya ukatili kwa sababu mahakama zilizopo zinachelewesha maamuzi wakati mwingine utakuta shahidi muhimu anaweza kufariki dunia ama kuhama na kutopatikana suala ambalo linafanya haki kutotendeka.
"Mimi nilifanyiwa ukatili na mwenza wangu mwaka 2020 kwa kikatwa mkono na hukumu imetoka mwaka jana kwa mhusika kufungwa na matukio ya ukatili kwa wanawake ni mengi sana kijijini naiomba serikali ikipendezwa ianzishe mahakama itakayoshughulika na masuala ya ukatili"
Ends
0 Comments