Mfanyabiashara maarufu wa maduka ya simu jijini Arusha aliyefahamika kwa jila moja la Mally amekutwa amekufa kwenye gari yake katika eneo la Maegesho ya Magari (CITY CAR WASH)mkabala na jengo la CCM Mkoa wa Arusha.
Askari polisi walifika eneo la tukio na kuukuta mwili huo uliokuwa kwenye gari aina ya SCUDO lenye namba T 466 AUB lililokuwa limeegeshwa katika eneo hilo .
Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa marehemu Mally amekuwa na tabia ya kufika eneo hilo na kuegesha gari lake na kisha kwenda bar iliyopo eneo hilo kwa ajali ya kula chakula na kunywa.
Mwenyekiti wa eneo hilo maarufu kwa wauzaji wa magari (madalali) ,Alex Kahela alisema alipata taarifa asubuhi ya leo oktoba 13, kuhusiana na tukio hilo na baada ya kufika aliweza kulitambua gari hilo kuwa ni mali ya mfanyabiashara huyo.
"Baada ya kupata taarifa nilifika eneo la tukio na kujaribu kuchungulia ndani ya gari hiyo lililokuwa limefungwa milango kwa ndani tukiwa na watu wengine tuligundua kuwa mwili uliopo ndani ni wa mzee Mally"
Alisema hafahamu chanzo cha kifo chake na mwili huo wanakadilia kuwa ndani ya gari hilo kwa siku mbili au tatu bila kughundulika hadi Leo harufu iliyokuwa ikitoka katika gari hilo iliwashtua watu hao la kuwalazimu kuoata na wasiwasi na gari hilo kabla ya kuamua kusogelea na kuchungulia.
Mwosha magari Juma jumapili alisema jana jioni walianza kusikia harufu huyo hata hivyo haikuwa kali sana na kujikuta wakiendelea na shughuli zao ila leo kwa sababu kumekucha na jua kali harufu iliongezeka na kuwa kali zaidi.
Shuhuda mwingine Peter Kivuyo alisema kuwa baada ya kusikia harufu kali waliaogelea gari hilo na walipochubgulia ndani ndipo walipogundua kuna mwili wa mtu akiwa haongei.
Alisema alipoutazama vizuri mwili huo aliweza kumtambua kuwa ni Mzee Mally huku pembeni ya mwili kukiwa na mabunda ya fedha na waliona michiriźi ya damu eneo la kifua.
"Niliuona mwili wa marehemu sehemu ya kifua kukiwa na michirizi ya damu huku pembeni akionekana ameshika mabunda ya fedha"
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Justine Masejo hakuweza kupatikana kuongelea tukio hilo na gari la marehemu liķiwa na mwili lilichukuliwa kwa kuvutwa na kupelekwa moshwale kwa ajili ya uchunguzi na kuhifadhi mwili huo.
Katika tukio hilo watu kadhaa walichukuliwa nankupelekwa kituo cha polisi kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.
Ends..
0 Comments